Natangaza nafasi ya kazi ya Muuzaji wa duka la bidhaa za ngozi na mwili.
Eneo la biashara ni Mikocheni, karibu na Mikocheni Plaza
Mshahara: 400,000 TZS kwa mwezi ( unaweza ongezeka kama utakuwa na ujuzi wa ziada wa kutumia kifaa Cha kupima ngozi)
Siku za Kazi: Jumatatu hadi Jumamosi, 3:30 asubuhi – 1:30 usiku.
Mapumziko: Jumapili na siku zote za sikukuu kubwa; Pasaka, Eid na Xmass.
SIFA ZA MWOMBAJI:
- Tunatafuta mtu mwenye bidii.
- Muaminifu wa Hali ya juu.
- Anayependa masuala ya ngozi na mwenye kujua bidhaa za ngozi na kazi yake.
- Mbunifu, mtu wa kujiongeza.
- Dependable and reliable.
- Kijana au mdada SMART, MSAFI, ANAYEJIPENDA na kupenda kazi yake.
- Anayejua kutumia kifaa Cha kupima ngozi, na kuweza kumsomea mteja majibu yake ya ngozi na kumpa ushauri wa bidhaa gani atumie.
MAJUKUMU YA KAZI:
- Kuuza bidhaa za ngozi na mwili kwa wateja.
- Kuwashauri wateja kuhusu bidhaa zinazofaa kwa changamoto zao za ngozi.
- Kutumia kifaa cha uchambuzi wa ngozi na kuwasaidia wateja.
- Kufanya usafi wa Duka na kuweka mpangilio wa duka vizuri.
- Kurekodi mauzo ya kila siku na kufanya hesabu ya bidhaa.
- Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na msimamizi.
SIFA ZINAZOHITAJIKA:
- Uelewa wa msingi wa bidhaa za ngozi na mwili.
- Uwezo wa Hali ya juu wa mawasiliano na kuhudumia wateja.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Kama unakidhi vigezo vilivyoainishwa na unavutiwa kujiunga na timu yetu, tafadhali tuma CV na passport size photo yako kwa Whatsapp namba 0787998926.
Leave a Reply