Wakati Fulani nilikua nahitaji vijana watatu kwa ajili ya kazi za graphics designing, marketing and secretary; hivyo nikatengeneza tangazo ambalo lilisambaa sana kwenye majukwaa ya mtandaoni hasa mitandao ya kijamii. Ndani ya muda wa wiki moja nilikua nimepokea maombi na cv Zaidi ya 70 za vijana wa kike na wa kiume wakijaribu bahati yao katika mojawapo ya kazi hizo tatu. Wingi wa zile CV pamoja na makosa yaliyokuwemo kwenye zile CV vikanisukuma kuandika Makala hii.

CV ni ufupisho wa maneno ya kilatini “curriculum vitae” yenye maana ya “life history” kwa kiingereza na kwa Kiswahili “historia ya Maisha” (wasifu). Hivyo kwa lugha nyepesi CV ni historia ya Maisha yako kwa ufupisho iliyoandikwa kwa namna ambayo itaonekana inafaa kwa ajili ya suala Fulani (hasa kazi mpya). Ni sehemu ambapo unatakiwa kutumia lugha nzuri, fupi na yenye kueleweka kujieleza.
- Mpangilio (layout)
Kuna layout (mipangilio) nyingi sana za muonekano wa jumla wa wasifu (CV). Kuhusu mipangilio hii ni juu yako kuchagua ule unaopendezwa nao wewe mwenyewe. Hapa ni suala la wewe kuona formula ipi unaona inakupendeza kimuonekano. Hakuna formula ya lazima ama ambayo ni bora kuliko zote. Cv yako lazima iwe na mpangilio mzuri ulio rahisi kueleeweka usio na vipengele vingi. Unapotuma maombi ya kazi mpya kumbuka si wewe tu unaetuma cv yako kwa huyo muajiri mpya, hivyo ungependa cv yako ndio iwe ya kuvutia kuliko zote machoni pa atakaeipitia na sio iishie kutupwa bila hata kusomwa kwa kina. Kila unachokiandika lazima kiwe cha kweli sio maelezo mengi ya kujaza tu kurasa.
- Vipengele
CV lazima iwe na vipengele angalau sita vya lazima. Navyo ni
- Profile Summary; Hapa unaweka maelezo mafupi kuhusu wewe mwenyewe. Namna ambavyo unaweza kujielezea hasa mawazo chanya na ujuzi wako ambao unaongeza sifa yako. Ni namna Fulani ya kufupisha sifa zako nzuri kwa ujumla pamoja na ujuzi na matarijio (objectives) yako katika kufanya kazi na kujiboresha.
- Personal particulars; haya ni maelezo yanyojibu kuhusu jina lako, tarehe ya kuzaliwa, anuani, kama una ndoa ama la, eneo unaloishi, mawasiliano na utaifa wako.
- Proffessional Experience; hii itaonyesha mahali ulipofanya kazi, majukumu uliyokuwa nayo pamoja na wakati gani (miaka). Kama ilivyo kwa maelezo ya elimu hapa pia ni lazima kuanza kueleza kwanza kazi, majukumu na mahali unapofanya kazi wakati huu na kuendelea kueleza kazi nyingine ulizowahi kufanya.
- Education Background; ni kipengele chenye mtiririko wa vyuo, shule pamoja na fani ulizozisomea. Ni lazima kuziandika kwa mtiririko wa kuanzia na elimu uliyoipata hivi karibuni na kumalizia na elimu au kozi ya kwanza kabisa bila kusahaauo muda (miaka).
- Other trainings; ni maelezo kuhusu mafunzo mengineyo uliyowahi kufanya. Kumbuka haya si mafunzo ya kitaaluma kama ilivyo kwa kipengele nammba tatu; haya ni mjumuisho wa semina au kozi fupi za kuongeza ujuzi ulizopitia.
- Referees; kama lilivyo neno lenyewe ‘marefarii’ hapa unaweka majina na mawasiliano ya watu watatu au wawili kulingana na mahitaji ya muajiri wako. Marefarii hawa ni watu ambayo wanakufahamu vizuri na hata muajiri wako mpya anaweza kuwapigia na kuwauliza kuhusu wewe wakampa maelezo ya kujitosheleza. Ni vyema ukawaweka watu ambao uliwahi kufanya nao kazi kwa mfano mwajiri wako aliyepita, au bosi wako katika idara uliyofanya kazi au mkuu wa idara mahali ulipowahi kujitolea kufanya kazi. Lakini kabla hujawaandika majina na mawasiliano yao katika CV yako ni vyema ukawataarifu kwanza kuhusu hilo.
Unaweza ukawa umekutana na mifano ya CV yenye vipengele Zaidi ya hivi vilivyotajwa hapa. Sio dhambi kuwa na vipengele Zaidi ya hivi. Angalizo ni kwamba chochote unachokiongezea kwenye CV ni sharti kiwe kinaongeza uzito wa CV yako sio maelezo marefu tu yasio na maana au yanayojirudiarudia.
- Muundo (Format)
Kuwa makini sana na suala hili la format. Mara nyingi imetokewa watu wakiandika CV zako na kuzituma (e-mail) katika muundo wa Microsoft word na zikifunguliwa tu mpangilio (layout) unaharibika. CV za mtindo huu huwa zinaishia kupuuzwa tu hata kama aliyetuma ni mtu sahihi kwa kazi hiyo. Kawaida tunaandika documenti zote katika format ya Microsoft word (yoyote ile, iwe ni yam waka 2003, 2007, 2010 au ya 2013). Kila ukifanya mabadiliko kumbuka kuzihifadhi katika muundo wa Microsoft word pamoja na muunda wa pdf (portable document file). Muundo wa Microsoft word utakusaidia kufanya mabadiliko wakati wowote na ukahifadhi na muundo wa pdf ndio unaopendelewa na watu wengi katika kutuma kwa intanenti. Kabla hujatuma CV yako soma maelezo muajiri wako anahitaji CV yako katika muundo upi. Kama anahitaji katika muundo wa Microsoft word (ambayo ni mara chache sana kutokea) jitahidi kuihifadhi CV yako katika format ya Microsoft word ya mwaka 2007 ili iwe rahisi kufunguka kwake. Lakini kama hakusema muundo wowote basi itume CV yako iliyohuishwa katika muundo wa PDF.
- Picha
Nimekutana na maswali mengi sana kuhusu umuhimu wa picha katika CV. Je, picha ni lazima iwepo kwenye CV? Jibu langu mara zote limekuwa ni; Picha ni muhimu japo si lazima. Si, kweli kwamba usipoambatanisha picha katika CV yako unakuwa umefanya makosa. Lakini ni muhimu kwa kuwa inaongeza sifa Fulani, katiak mpangilio na maelezo yako. Kitu cha msingi cha kufuatilia katika uwekaji wa picha ni mpangilio tu. Iweke picha yako ya hivi karibuni katika mpangilio unaopendeza.
- Uhuhishaji (Updating)
Kama kilivyo kipengele cha format ya CV yako, kipengele hiki cha uhuhishaji wa CV yako kina umuhimu pia. Uhuhishaji ni kufanya mabadiliko katika CV yako kwa kuongeza maelezo Zaidi katika vipengele vya CV yako. CV yako ya miaka kumi iliyopita haiwezi kuwa sawa na CV yako ya mwaka huu. Usiitume CV yako kwa muajiri mpya kablya kuipitia na kufanya mabadiliko.
Lakini pia kumbuka CV haitakiwi kuwa na kurasa nyingi angalau kurasa mbili zinatosha na inapobidi basi kurasa tatu mwisho.
Bofya hapa ili kupakua mfano wa CV.
KUMBUKA
Muajiri au huyo ambaye ataisoma hiyo CV yako vitu vitatu vya muhimu anavyovihitaji ni elimu ya fani Fulani uliyonayo, uzoefu wa kazi na ujuzi unaoambatana na kazi hiyo mpya. Akivutiwa na vitu hivi moja kwa moja atatazama jina lako na labda kuamua kuwasiliana nawe. Namna hii unakua umeibuka kinara katika mamia au hata maelfu ya CV Zilizotumwa. Kamwe usimtumie mtu mwingine kukuandikia CV yako. Kwa kuwa ni wewe tu ndio unaweza kujieleza kwenye hayo maandishi ya CV yako huku ukiendana na matakwa (requirements) ya muajiri mpya. Hatari ya kuandikiwa CV inakuja pale ambapo mwajiri mpya ataamua kukuuliza maswali kutokana na maelezo uliyoyaandika kwenye CV. (Sasa kama hukuandika mwenyewe wala kuipitia hiyo CV baada ya kuandikiwa ukaamua kuamini katika maelezo ya huyo anayefanya biashara ya kuandikia watu CV utashindwa kujibu maswali hasa yale ya kimitego kuhusu CV yako). Hatari nyingine ni kwamba mameneja waajiri wana uzoefu mwingi kiasi cha kutambua haraka CV iliyoandikwa na mhusika mwenyewe au iliyotengenezwa na watu au machine. Kumbuka kutuma CV yako katika format ya PDF kama hakuamrishwa kutuma katika format yoyote.
Muandishi wa Makala hii ni kijana mjasiriamali wa biashara na mambo ya mawasiliano. Ana uzoefu wa miaka 10 ya uandishi wa Makala mbalimbali. Pia ni mzoefu katika kusimamia Biashara. Kwa sasa ni Meneja wa Hoteli ya Kitalii huko Zanzibar na Katibu wa vikundi hiari. Anatoa ushauri juu ya maswala mbalimbali,anahusika na kuunganisha waajiri na wanaotafuta kazi na pia kuunganisha watu wa kada tofauti katika kuzitambua fursa, kuzinyaku fursa, na kujipatia nafasi katika mnyororo wa thamani. Anapatikana kwa: +255 776 441 991, matona@nkosiwaafrika.com
Leave a Reply